Habari Za Un
19 FEBRUARI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:09:55
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu nchini DRC, na simulizi y amkimbizi wa DRC aliyekimbilia nchini Uganda. Makala inatupeleka nchini Tanzania, namashinani nchini Kenya, kulikoni?Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya kikao cha dharura jijini New York, Marekani kujadili hali ya usalama inayozidi kuzorota kila uchao huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya kibinadamu nchini humo, Bruno Lermaquis amesema kupanuka kwa mzozo huo kumezidi kugharimu maisha na mustakabali wa raia.Sina mpango tena wa kurejea nyumbani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ni kauli yake Twagirayesu Gato, mwanafunzi huyu raia wa DRC aliyekimbia nchini mwake mwaka jana na kuingia Uganda ambako sasa anapata hifadhi. Amesema hayo kwenye video ya shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR iliyochapishwa katika ukurasa wa YouTube wa shirika hilo.Makala inatupeleka nchini Tanzania ambako tunamsikiliza Brigedia Jenerali George Mwita Itang’ar