Habari Za Un

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 8:29:30
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • Maji ni Uti wa mgongo kwa jamii kote duniani - Stephen Tai

    28/08/2025 Duración: 05min

    Wiki ya Maji ikifikia tamati leo Agosti 28 na maudhui yakiwa Maji kwa ajili ya Hatua kwa Tabianchi, tunabisha hodi kaunti ya Kajiado nchini Kenya kumsikia mtendaji kwenye mradi wa maji wa Kerarapon Water Association  ambalo ni shirika la kijamii linalohusika na maji na mazingira huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Mtendaji huyo anayeanza kwa kujitambulisha, anazungumza na Kelvin Keitany wa radio washirika Radio Domus nchini Kenya.

  • Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MKWIJI!.

    28/08/2025 Duración: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWIJI! 

  • 28 AGOSTI 2025

    28/08/2025 Duración: 09min

    Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina, wiki ya Maji ikifikia tamati leo Agosti 28 na maudhui yakiwa Maji kwa ajili ya Hatua kwa Tabianchi, tunabisha hodi kaunti ya Kajiado nchini Kenya kumsikia mtendaji kwenye mradi wa maji wa Kerarapon Water Association  ambalo ni shirika la kijamii linalohusika na maji na mazingira huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Mengine ni kama yafuatayo.Ukraine ambapo leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameungama na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kulaani vikali mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani droni yaliyofanywa na Urusi usiku kucha kuamkila dhidi ya miji ya Ukraine na kusababisha vifo na majeruhi kwa raia, wakiwemo watoto, na pia kuharibu majengo ya kidiplomasia jijini Kyiv. Amesisitiza kuwa mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu yao yanakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu, akitaka yakome mara moja na kurudia wito wake wa kusitisha mapigano ili kuelekea amani ya kudumu itakayoheshimu uhuru wa watu, uhuru wa kitaifa na mipa

  • Mradi wa MONUSCO kwa ushirikiano na PAMI waleta nuru kwa wakazi Nyiragongo, DRC

    27/08/2025 Duración: 04min

    Kwa zaidi ya muongo mmoja, eneo la Nyiragongo lililoko jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) limekumbwa na hali ya kutokuwepo kwa utulivu wa kudumu kutokana na uwepo wa makundi yenye silaha. Maelfu ya familia wamekimbia makazi yao na watoto wengi kulazimishwa kujiunga na makundi hayo ya kijeshi. Kati ya mwaka 2024 na 2025, kuzuka upya kwa mapigano kunakohusishwa na kuibuka tena kwa waasi wa M23 kumeongeza zaidi hali ya hatari kwa wakazi wa eneo hilo, hasa watoto na vijana. Ili kuleta ahueni kwa wakazi, Umoja wa Mataifa umechukua hatua. Je ni zipi hizo? Ungana basi na Anold Kayanda kwenye makala hii.

  • Leo ni siku ya Ziwa, wakazi wa Ziwa Victoria wapaza sauti ya faida zake

    27/08/2025 Duración: 01min

    Leo ni maadhimisho ya kwanza ya siku ya Ziwa Duniani yakibeba maudhui "Ziwa ni uti wa mgongo wa sayari yetu" na ili kuthibitisha hilo tunakupeleka  Mwanza Kaskazini Magharibi mwa Tanzania ambako , Bosco Cosmas kutoka Radio washirika SAUT FM anamulika maoni ya wananchi ni kwa vipi ziwa Victoria limekuwa msaada na mkombozi kwao.

  • Afisa wa UN ajionea jinsi Tanzania 'inafunda' waendao kwenye operesheni za ulinzi wa amani

    27/08/2025 Duración: 02min

    Mratibu Maalum wa Kuboresha Hatua za Umoja wa Mataifa dhidi ya Unyanyasaji wa kingono (SEA) Christian Saunders amefanya ziara nchini Tanzania kuona maandalizi ya vikosi vya operesheni za ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania, Kapteni Mwijage Inyoma Afisa Habari wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) ametuandalia taarifa hii.Ni bendi ya jeshi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ ikiongoza askari wengine kumkaribisha Bwana Christian Saunders hapa katika Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) Kunduchi, Dar es Salaam.Miongoni mwa askari hawa tayari wameandaliwa kwenda katika nchi mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hata nje ili kuusaidia Umoja wa Mataifa kutekeleza moja ya majukumu yake kwa ulimwengu, kuleta na kuitunza amani.Bwana Saunders anasema, “wacha nianze kwa kusema asante. Kusema asante ni jambo muhimu sana, kwa sababu mko tayari kuanza jukumu la kutumwa, iwe mnaenda Lebanon au Jamhuri ya Kidemokrasia y

  • 27 AGOSTI 2025

    27/08/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika maadhimisho ya siku ya Ziwa duniani; Maandalizi ya walinda amani kwenda kuhudumu CAR ma DRC; Msaada wa MONUSCO kwa wakazi wa Kivu Kaskazini; Aliyerejesha fadhila kwa WFP.Leo ni maadhimisho ya kwanza ya siku ya Ziwa Duniani yakibeba maudhui "Ziwa ni uti wa mgongo wa sayari yetu" na ili kuthibitisha hilo tunakupeleka  Mwanza Kaskazini Magharibi mwa Tanzania ambako , Bosco Cosmas kutoka Radio washirika SAUT FM anamulika maoni ya wananchi ni kwa vipi ziwa Victoria limekuwa msaada na mkombozi kwao.Mratibu Maalum wa Kuboresha Hatua za Umoja wa Mataifa dhidi ya Unyanyasaji wa kingono (SEA) Christian Saunders amefanya ziara nchini Tanzania kuona maandalizi ya vikosi vya operesheni za ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania, Kapteni Mwijage Inyoma Afisa Habari wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) ametuandalia taarifa hii.Anold Kayanda anatupeleka eneo la Maziwa Makuu barani Afrika kusikia

  • 26 AGOSTI 2025

    26/08/2025 Duración: 09min

    Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakulatea-Ripoti mpya kwa jina Maendeleo katika Maji ya Kunywa na Kujisafi Majumbani iliyozinduliwa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa imeonesha kwamba, licha ya hatua kupigwa, mtu 1 kati ya 4 duniani bado hana upatikanaji wa maji salama ya kunywa. -Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imetoa wito kwa mamlaka za Misri kukomesha mfumo wa “mzunguko” unaofanya wakosoaji wa Serikali kuzuiliwa kiholela na kwa muda mrefu, hata baada ya kumaliza vifungo vyao. - Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi,UNHCR leo limepongeza Serikali ya Kifalme ya Thailand kwa kupitisha azimio litakalowapa wakimbizi wa muda mrefu kutoka Myanmar haki ya kufanya kazi nchini Thailand.-Katika mada kwa kina tunamulika uzinduzi wa shule ya kwanza ya Akili Mnemba iliyoanzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women huko ukanda wa Asia na Pasifiki-Na mashinani utamsikia Ibrahim Al-Najjar mkimbizi huko Ukanda wa

  • Gaza: Mtoto mwenye umri wa miaka 11 ana uzito wa kilo 9, kisa njaa!

    25/08/2025 Duración: 03min

    Baada ya miaka miwili ya vita katika Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel Ijumaa tarehe 22 Agosti Umoja wa Mataifa ukatangaza jambo baya zaidi, ripoti ya njaa duniani IPC ikathibitisha wananchi wa Gaza rasmi wana kabiliwa na baa la njaa.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP ni moja kati ya mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo pamoja na hali ya vita yamekuwa yakitoa msaada wa chakula huko Gaza na wameeleza kwamba baa la njaa lazima likomeshwe kwa gharama yoyote ile. Kusitishwa kwa mapigano mara moja na kukomesha mzozo ni muhimu ili kuruhusu misaada kuweza kuingizwa  Gaza ili kuokoa maisha. Makala hii Leah Mushi anamuangazia mmoja wa watoto wanaokabiliwa na njaa

  • Tangu 2017 hadi leo warohingya wanahaha bila kujua mustakabali wao

    25/08/2025 Duración: 01min

    Leo Agosti 25 ni miaka minane tangu kufurushwa kwa wingi watu wa kabila la Rohingya kutoka katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar. Umoja wa Mataifa unatoa wito wa mshikamano wa kimataifa kuwasaidia kwani mateso kwa watu hao yanaendelea kuwa mabaya zaidi kila uchao. Anold Kayanda na taarifa zaidi.Asante AssumptaMyanmar (zamani ikiitwa Burma) ni nchi ya Kusini Mashariki mwa Asia yenye zaidi ya makabila 100, inayopakana na India, Bangladesh, China, Laos na Thailand.Warohingya wanafurushwa na kuteswa kwasababu mbalimbali zikiwemo za kihistoria kwa madai kuwa walitoka Bangladesh ingawa wameishi vizazi na vizazi nchini Myanmar. Pia sababu ya imani yao kwa uislamu miongoni mwa sababu nyingine.Ni miaka minane sasa tangu ufurushwaji mkubwa wa jami hii kutoka jimbo la Rakhine pwani ya Magharibi mwa Myanmar. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anaonya kuwa Warohingya na raia wengine bado wanakabiliwa na ukiukaji wa haki za binadamu na kufurushwa. Anaeleza wasiwasi wake kuhusu tarifa za kufukuzwa na kupunguz

  • Apoteza mwanae akikimbia machafuko

    25/08/2025 Duración: 02min

    Machafuko yanayoendelea Kaskazini Mashariki mwa Burkina Faso yamefurusha maelfu ya watu, kukatili maisha na kuwalazimisha wengi kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao. Miongoni mwa simulizi za kugusa ni ya Fadima Bandé mama aliyelazimika kufungasha virago kunusuru maisha yake na wanawe wawili lakini akaishia kupoteza mmoja, je ilikuwaje?  kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Flora Nducha anasimulia zaidi.Katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Dori Mashariki mwa Burkina Faso, sasa ni maskani ya Fadima, maisha hapa ni magumu na hana tena njia ya kujipatia kipato. Kila uchao analazimika kupambana kuhakikisha watoto wake wanapata angalau mahitaji ya msingi, anakumbuka safari ya uchugu kutoka Kijiji kwake Sohlan hadi hapaWakati tunakimbia mmoja wa binti zangu mapacha aliugua baada ya kunyeshewa na mvua kubwa na kupata mafua makali, wakati tayari alikuwa anaumwa utapiamlo. Tulimkimbiza hospitai mjini Sebba lakini akafariki dunia.”Baada ya kupata hifadhi kambini Dori Fadima akajaliwa

  • 25 AGOSTI 2025

    25/08/2025 Duración: 09min
  • Afrika bado inaathirika kwa kiwango kikubwa, na kwa sasa inakumbwa na Ugaidi - Guterres

    22/08/2025 Duración: 03min

    Tarehe 18 Agosti mwaka 2025 siku ya Jumatano, wajumbe 15 wa Baraza la Usalama walikutana kujadili Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kikundi cha kigaidi cha ISIL/Da’esh.Walikabidhiwa ripoti hiyo ya 21 ikimulika vitisho vinavyotokana na kikundi hicho ambacho kirefu chake ni Islamic State in Iraq and the Levant au pia Da’esh. Ripoti ikigusia tishio la kikundi hicho katika maeneo mbalimbali duniani, lakini makala hii initajikita zaidi barani Afrika!

  • 22 AGOSTI 2025

    22/08/2025 Duración: 11min

    Jaridani leo tunaangazia baa la njaa katika ukanda na huduma za afya katika ukanda wa Gaza. Makala tunafuatilia harakati dhidi ya ugaidi ukimulika ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na mashinani tunaangazia simulizi za wakimbizi kupitia vyombo vya habari.Zaidi ya nusu milioni ya watu huko Gaza wameripotiwa kukumbwa na baa la njaa, hali ambayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameielezea kuwa “janga lililosababishwa na mwanadamu, shutuma ya kimaadili na kushindwa kwa ubinadamu.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, licha ya mazingira magumu linaendelea na juhudi za kuokoa uhai wa kila binadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza linalokaliwa kimabavu na Israel. Wakati huo huo linatoa wito kwa mataifa mengine kufuata mfano wa Umoja wa Falme za kiarabu, UAE ambao juzi Jumatano wamewapokea baadhi ya wagonjwa mahututi na majeruhi waliobahatika kuhamishwa Gaza ili kupata huduma za kiafya wanazozihitaji.Katika makala Assumpta Massoi anamulika Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Matai

  • WHO: Mataifa mengine tafadhali fuateni mfano wa UAE kupokea wagonjwa kutoka Gaza

    22/08/2025 Duración: 02min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, licha ya mazingira magumu linaendelea na juhudi za kuokoa uhai wa kila binadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza linalokaliwa kimabavu na Israel. Wakati huo huo linatoa wito kwa mataifa mengine kufuata mfano wa Umoja wa Falme za kiarabu, UAE ambao juzi Jumatano wamewapokea baadhi ya wagonjwa mahututi na majeruhi waliobahatika kuhamishwa Gaza ili kupata huduma za kiafya wanazozihitaji. Anold Kayanda anaeleza anawaangazia baadhi yao.

  • Baa la njaa kuthibitishwa Gaza, Guterres asema, huku ni kushindwa kwa ubinadamu

    22/08/2025 Duración: 01min

    Zaidi ya nusu milioni ya watu huko Gaza wameripotiwa kukumbwa na baa la njaa, hali ambayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameielezea kuwa “janga lililosababishwa na mwanadamu, shutuma ya kimaadili na kushindwa kwa ubinadamu.”Flora Nducha na taarifa zaidi

  • 21 AGOSTI 2025

    21/08/2025 Duración: 09min

    Nchini Tanzania Programu ya Pamoja ya Kigoma, (KJP) inayotekelezwa kwenye mkoa huo ulioko magharibi mwa Tanzania kwa lengo la kujengea uwezo wa kuhimili changamoto zitokanazo na uwepo wa wakimbizi unaendelea kujengea uwezo wenyeji na hivi karibuni zaidi ni mradi wa kuongezea thamani zao la alizeti. Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi anakupasha zaidi.

  • Ukanda wa Gaza unaongoza duniani kwa watu waliokatika viungo

    20/08/2025 Duración: 02min

    Maelfu ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ambao wamepoteza viungo vyao vya mwili na wanakabiliwa na hali mbaya ya maisha na matatizo makubwa ya kiafya kutokana na ukosefu wa huduma bora za matibabu na viungo bandia wanazohitaji sana. Anold Kayanda na taarifa zaidi.

  • Ukatili wa kijinsia katika mizozo

    20/08/2025 Duración: 03min

    Msikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa leo tunakuletea makala yenye kugusa maisha ya maelfu ya watu kote duniani, ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 19 Agosti limekutana jijini New York Marekani kujadili hali hii inayozidi kuongezeka, na kushuhudia jinsi waathirika wanavyobaki bila msaada wa kutosha kutokana na ukosefu wa rasilimali.Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa na Mwakilishi wake imeonesha ongezeko kubwa la kesi za ukatili wa kingono, jambo linaloibua maswali makubwa kuhusu uwajibikaji na huduma kwa manusura. Leah Mushi ametuandalia makala ifuatayo ikieleza hayo kwa kina.

  • 20 AGOSTI 2025

    20/08/2025 Duración: 09min

    Jaridani leo tunaangazia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, na hali ya kibinadamu Gaza na majeraha kwa wenyeji. Makala tunaangazia ukatili wa kingono na mashinani tunakwenda Sudan kumulika jinsi wanavyokabiliwa na unyanyasaji huo wa kingono.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema Afrika inahitaji mageuzi makubwa ya Baraza la Usalama na mfumo wa kimataifa wa fedha ili kufanikisha maendeleo yake na nafasi yake duniani. Akihutubia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, Guterres ameweka vipaumbele vitano.Maelfu ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ambao wamepoteza viungo vyao vya mwili na wanakabiliwa na hali mbaya ya maisha na matatizo makubwa ya kiafya kutokana na ukosefu wa huduma bora za matibabu na viungo bandia wanazohitaji sana.Tunakuletea makala yenye kugusa maisha ya maelfu ya watu kote duniani, ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 19 Agosti limekutana jijini New York Marekani ku

página 1 de 5