Habari Za Un
Apoteza mwanae akikimbia machafuko
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:02:25
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Machafuko yanayoendelea Kaskazini Mashariki mwa Burkina Faso yamefurusha maelfu ya watu, kukatili maisha na kuwalazimisha wengi kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao. Miongoni mwa simulizi za kugusa ni ya Fadima Bandé mama aliyelazimika kufungasha virago kunusuru maisha yake na wanawe wawili lakini akaishia kupoteza mmoja, je ilikuwaje? kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Flora Nducha anasimulia zaidi.Katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Dori Mashariki mwa Burkina Faso, sasa ni maskani ya Fadima, maisha hapa ni magumu na hana tena njia ya kujipatia kipato. Kila uchao analazimika kupambana kuhakikisha watoto wake wanapata angalau mahitaji ya msingi, anakumbuka safari ya uchugu kutoka Kijiji kwake Sohlan hadi hapaWakati tunakimbia mmoja wa binti zangu mapacha aliugua baada ya kunyeshewa na mvua kubwa na kupata mafua makali, wakati tayari alikuwa anaumwa utapiamlo. Tulimkimbiza hospitai mjini Sebba lakini akafariki dunia.”Baada ya kupata hifadhi kambini Dori Fadima akajaliwa