Habari Za Un

08 MEI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa ambayo Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na kiongozi wa kijamii kutoka Jamii ya wafugaji ya Wamaasai mkoani Morogoro nchini Mashariki mwa Tanzania Adam Kulet Ole Mwarabu.Wiki kumi baada ya kuanza kwa mzingiro kamili wa Israel dhidi ya wakazi wa Gaza, zaidi ya robo tatu ya kaya katika eneo la Palestina kuna uhaba mkubwa wa huduma ya maji, huku hali ya usafi ikizidi kuwa mbaya, yameonya leo mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu athari za "uhaba huo wa maji kwa kuzingatia kuwa msimu wa joto unakaribia.”Ripoti kutoka Sudan zikidai kwamba juzi jumatano kulikuwa na jaribio la mashambulizi mapya ya ndege zisizo na rubani dhidi ya kitovu muhimu cha misaada nchini humo juzi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia tamko alilolitoa jana jioni kwa saa za New York, Marekani, ameongeza nguvu yake katika kutoa wito unaozidi kuwa wa muhimu kuhamasisha kuanzishwa kwa mazungumzo ya amani ya kweli.Kufuati