Habari Za Un

07 MEI 2025

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunaangazia mvutano unaoendelea barani Asia kati ya majirani wawili India na Pakistani, na msaada wa mguu bandia uliowezesha mtototo nchini Kenya kwenda shule. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani tunakwenda katika ukanda wa Gaza.Huko barani Asia majirani wawili India na Pakistani wameendelea kuoneshana mvutano kati yao kwenye eneo la Jammu na Kashmiri tangu tarehe 22 mwezi uliopita wa Aprili baada ya shambulizi huko Pahalgam. Katibu Mkuu ametoa wito kwa mara nyingine tena.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau wameleta neema kwa watoto wanaoishi na ulemavu katika Kaunti ya Kisumu Magharibi mwa Kenya baada ya kuwapa msaada wa vifaa ikiwemo viti mwendo na viungo bandia kupitia mradi wa ubunifu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, msaada uliobadili maisha yao.Makala katika wiki ya chanjo duniani, iliyotamatishwa tarehe 30 wiki iliyopita, mtaa wa Butiama, ulioko Mtoni Kijichi katika wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania ulishu