Habari Za Un
06 MEI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:12:03
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha hapa makao makuu ambako Idhaa hii Dokta Willis Ochieng kutoka Kenya aliyehudhuria ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya kilimo na maendeleo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari, na mashinani tunakwenda Ghana.Ukuaji wa maendeleo ya binadamu – yanayopimwa kwa uhuru na ustawi wa watu – umeendelea kuwa wa kasi ndogo tangu mshtuko mkubwa wa janga la COVID-19 lakini kuna matumaini makubwa kwamba Akili Mnemba au AI, ikiwa itatumika kwa njia sahihi, inaweza kuwa chombo chenye nguvu cha kuboresha maisha ya mamilioni ya watu. Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya kila mwaka ya Maendeleo ya Binadamu iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP.Kulengwa kwa hospitali ya Médecins Sans Frontières nchini Sudan Kusini kunaweza kuwa uhalifu wa kivita imeeleza leo Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu Sudan Kusini kufuatia mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa dhidi ya