Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Robert Francis Prevost achaguliwa kumrithi Papa Francis na kuchukua jina la Papa Leo XIV

Informações:

Sinopsis

Makala haya yanaangazia taarifa mbalimbali ikiwemo, Mmarekani Robert Francis Prevost, achaguliwa kuongoza kanisa katoliki duniani, akichukua jina la Papa Leo wa kumi na nne. Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, chatumbukia katika sintofahamu zaidi kufuatia baadhi ya waliokuwa wajumbe wa kamati kuu ya chama, kutangaza kujiondoa kwenye chama hicho. Tarifa zingine utakazoskia, silaha za China zilizoagizwa na taifa la Falme za Kiarabu zimepatikana zikitumika na wapiganaji wa RSF nchini Sudan, na nchi jirani za India na Pakistan zashambiliana kwa silaha nzito na kuzua wasiwasi mkubwa katika maeneo ya mipakani.