Jukwaa La Michezo

Droo ya CHAN 2024: Kenya yapangwa kundi gumu zaidi, mashindano ya Agosti 2025

Informações:

Sinopsis

Kipindi cha leo kimeangazia pakubwa droo ya mashindano ya CHAN 2024; adhari ya kuahirishwa kwa kipute na uchambuzi wa makundi. Pia tumetupia jicho raundi ya sita hatua ya makundi mechi za klabu bingwa Afrika, fainali ya mashindano mapya ya wasichana U17, Shujaa yataja kikosi chake cha mkondo wa Perth 7s, Kipchoge akilenga taji la tano la London Marathon, Tyson Fury astaafu ndondi kwa mara ya pili pamoja na mashindano ya tenisi ya Australian Open yakiingia hatua ya robo fainali. Kulingana na droo iliyofanyika Jumatano usiku katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi nchini Kenya, Harambee Stars imepangwa katika 'kundi la kifo' ambapo itamenyana na mabingwa mara mbili Morocco (2018 na 2020) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (2009 na 2016)."Tuko kwenye kundi la kifo," Mariga alikiri, akibainisha uimara wa wapinzani wao."Hizo ni timu kubwa na inamaanisha lazima tuweke juhudi zaidi katika maandalizi."“Wapinzani wetu ni wagumu, tutashiriki mashindano haya kwa mara ya kwanza lakini ha