Sinopsis
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Episodios
-
Kenya: Nani atatamba kwenye "Debi ya Mashemeji" AFC Leopards vs Gor Mahia?
29/03/2025 Duración: 23minMiongoni tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo ya raga mkondo wa HongKong 7s, sakata la upangaji mchezaji dhidi ya golikipa wa Kenya Patrick Matasi, maandalizi ya debi ya Mashemeji, Misri yapewa haki za kuandaa AFCON U20 huku CAF ikiifungulia uwanja wa Benjamin Mkapa, tuzo nono kwa washindi wa Kombe la Dunia la vilabu, kocha wa Brazil atimuliwa naye Djokovic akikaribia kushinda taji lake la 100.
-
Mashindano ya kukimbiza magari, yapamba moto nchini Kenya
22/03/2025 Duración: 23minMashindano ya dunia ya kukimbiza magari, Safari Rally yanaendelea nchini Kenya. Madereva mbalimbali kutoka duniani, wanakutana mjini Naivasha kwa ajili ya kutafuta ubingwa wa mwaka 2025.
-
CAF: Motsepe achanguliwa tena kuwa rais kwa muhula wa pili wa miaka minne
15/03/2025 Duración: 23minTuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na uchaguzi wa CAF, uwanja wa Mkapa wafungiwa kwa muda, michuano ya kufuzu dimba la dunia kwa kina dada chini ya umri wa miaka 17, maandalizi ya mashindano ya kuendesha magari ya WRC Safari Rally, uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya hatua ya kumi na sita bora naye Neymar alazimika kuaga kikosi cha Brazil kufuatia jeraha
-
Misri, Morocco,Tunisia zang'ara mashindano ya tenisi ya vijana chini ya miaka 14
02/03/2025 Duración: 23minTuliyokuandalia hii leo ni pâmoja na matokeo ya mashindano ya tenisi ya vijana barani Afrika chini ya miaka 14, kocha mpya wa Kenya ni nani, matokeo ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada, timu sita kushiriki ligi ya Afrika ya basketboli kwa mara ya kwanza, huku Afrika Kusini ikijiandaa kutuma ombi rasmi la kuandaa mkondo mmoja wa F1 na Jose Mourinho apata afueni baada ya adhabu yake kupunguzwa.
-
Simba kukutana na Al Masry kwenye Droo ya robo fainali Kombe la Shirikisho CAF
22/02/2025 Duración: 23minTuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na matokeo kwenye mashindano ya kimataifa ya gofu ya Magical Kenya Open, bondia wa DRC kupambana na muingereza huko Saudi Arabia, maandalizi ya Tour du Rwanda, Droo ya robo fainali michuano ya klabu bingwa Afrika, mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada 2026 na basketboli ya 2025, halikadhalika Droo ya 16 bora mechi za klabu bingwa Ulaya na michuano ya raga ya Vancouver 7s.
-
Gofu: Wachezaji 150 kutoka mataifa 30 duniani kushiriki Magical Kenya Open 2025
15/02/2025 Duración: 23minTuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na taarifa kuelekea mashindano ya gofu duniani ya Magical Kenya Open 2025, bodi ya Ligi ya soka nchini Tanzania yashusha rungu kwa Pamba Jiji na Ally Kamwe, timu 18 zimehakikisha kushiriki mashindano ya voliboli ya ukanda wa tano nchini Uganda, droo ya michuano ya Afcon U17 na U20, mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya kina dada 2026, Jannik Sinner akubali kufungiwa miezi mitatu, raundi ya mtoano mechi za klabu bingwa Ulaya.
-
AFCON 2025: Uganda, Tanzania kundi moja katika mashindano ya mwezi Disemba
01/02/2025 Duración: 23minHii leo tumeangazia yaliyozungumziwa kwenye mkutano mkuu wa jinsia wa Afrika Mashariki jijini Nairobi, shirikisho la kimataifa la mchezo wa baiskeli yapinga madai kuwa Rwanda itapokonywa haki za kuandaa mashindano ya chipukizi ya dunia mwezi Septemba kufuatia mzozo unaoendelea DRC, uchambuzi wa droo ya AFCON 2025, maandalizi ya CHAN 2024 tarehe mpya zatajwa na uchaguzi wa CAF mwaka huu. Pia tumechabua hatua ya mchujo mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya na tetesi za uhamisho ulaya.
-
Ligi kuu ya Tanzania bara imetajwa nafasi ya nne barani Afrika na 57 duniani
25/01/2025 Duración: 23minJioni hii kwenye makala ya Jukwaa la Michezo tumeangazia Congo kufutiliwa kushiriki mashindano ya CHAN 2024, kufutwa kazi kwa kocha wa Rwanda Torsten Spittler, uwanja mpya wa Talanta jijini Nairobi unaendelea kupiga hatua kwenye ujenzi huku ligi ya Tanzania ikitajwa nafasi ya nne katika orodha ya ligi bora Afrika, Kenya yang'ara mashindano ya chipukizi ya tenisi, msururu wa raga ya dunia mkondo wa tatu, fainali za Australian Open na tetesi za uhamisho ulaya na Afrika.
-
Droo ya CHAN 2024: Kenya yapangwa kundi gumu zaidi, mashindano ya Agosti 2025
18/01/2025 Duración: 23minKipindi cha leo kimeangazia pakubwa droo ya mashindano ya CHAN 2024; adhari ya kuahirishwa kwa kipute na uchambuzi wa makundi. Pia tumetupia jicho raundi ya sita hatua ya makundi mechi za klabu bingwa Afrika, fainali ya mashindano mapya ya wasichana U17, Shujaa yataja kikosi chake cha mkondo wa Perth 7s, Kipchoge akilenga taji la tano la London Marathon, Tyson Fury astaafu ndondi kwa mara ya pili pamoja na mashindano ya tenisi ya Australian Open yakiingia hatua ya robo fainali. Kulingana na droo iliyofanyika Jumatano usiku katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi nchini Kenya, Harambee Stars imepangwa katika 'kundi la kifo' ambapo itamenyana na mabingwa mara mbili Morocco (2018 na 2020) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (2009 na 2016)."Tuko kwenye kundi la kifo," Mariga alikiri, akibainisha uimara wa wapinzani wao."Hizo ni timu kubwa na inamaanisha lazima tuweke juhudi zaidi katika maandalizi."“Wapinzani wetu ni wagumu, tutashiriki mashindano haya kwa mara ya kwanza lakini ha
-
CHAN 2024: Uwanja wa Nyayo nchini Kenya waidhinishwa na CAF kuandaa mashindano
11/01/2025 Duración: 23minTuliyokuandalia jioni hii ni pamoja na uchambuzi wa mashindano ya Mapinduzi, tetesi za uhamisho Afrika Mashariki, raundi ya tano ya mechi za klabu bingwa Afrika, maandalizi ya CHAN 2024, uhamisho wa wachezaji ulaya na mashindano ya tenisi ya Australian Open.
-
KENYA: Kuzaliwa, kufa na "kujaribu" kufufuka kwa mchezo wa masumbwi nchini Kenya.
08/01/2025 Duración: 38minPopote pale ulipo nikukaribishe katika Makala ya jukwaa la michezo ndani ya FRI Kiswahili.Leo tumekuandalia Makala spesheli ambayo inaangazia kushuka pakubwa kwa viwango vya mchezo wa masumbwi nchini Kenya, Makala ambayo tunayapeperusha wiki kadhaa tu baada ya kukamilika kwa michezo ya Olimpiki Jijini Paris nchini Ufaransa. Kwa mara ya kwanza katika, historia ya kenya, hakuna bondia hata mmoja aliyewakilisha taifa katika michezo ya olimpiki jijini Paris. Hatua hii ilizua ngumzo kwa wadau wa mchezo huo.Lakini, Iweje mchezo uliokuwa ukisifika na kuiletea Kenya hadhi katika miaka ya nyuma imedidimia kiasi hiki? Je, ni usimamizi mbaya ama ni ukosefu wa ligi dhabiti au ni kukosa wadhamini wa kuwekeza katika mchezo hili kuiletea fahari inayostahili. Je, Kuna uhasama kati ya wadau ama wasimamizi wameingiwa na kiburi na kujisahau na kuwasahau mabondia?Mwenzangu George Ajowi amezungumza na Mabondia wa zamani, marefa, makocha, mapromota, wanahabari na vile vile wadau wengeni katika sekta hii na kuzungumza nao kuhusiana
-
Mashindano ya magari ya Dakar Rally 2025 yang'oa nanga huko Saudi Arabia
04/01/2025 Duración: 23minLeo kwenye makala ya kwanza kabisa ya Jukwaa la Michezo mwaka 2025, tumeangazia raundi ya nne hatua ya makundi mechi za Ligi ya vilabu bingwa Afrika. Mwanariadha mkenya Beatrice Chebet avunja rekodi yake ya dunia huku raia wa Eritrea mwendesha baiskeli Biniam Girmay akishinda tuzo la Afrika wakati uo huo mashindano ya magari ya Dakar Rally na Kombe la Mapinduzi yaking’oa nanga. Lakini pia tutatupia jicho tetesi za uhamisho ulaya na michuano ya tenisi ya Brisbane Open inayoendelea.
-
CAF: Niger, Sudan na Zambia zafuzu mashindano ya soka ya CHAN 2024
28/12/2024 Duración: 23minIkiwa Jumamosi ya mwisho ya mwaka 2024, tunakuuliza ni tukio gani au mashindano gani ya kispoti yalikufurahisha zaidi mwaka huu? Pamoja na hayo; tumeangazia kifo cha mchezaji nguli wa voliboli nchini Kenya Janet Wanja, Uganda yaibuka mabingwa wa CECAFA michuano ya kufuzu AFCON U17, raundi ya mwisho ya kufuzu michuano ya CHAN 2024, uchambuzi wa raundi ya 18 ya mechi za Ligi Kuu ya Soka nchini Uingereza.
-
CHAN 2024: Rais Motsepe aridhishwa na maandalizi ya Kenya, Uganda na Tanzania
21/12/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa ziara ya rais wa CAF Patrice Motsepe Afrika Mashariki kuukagua maandalizi ya CHAN 2024, tuzo za wanasoka bora Afrika na FIFA mwaka huu, pigano la ndondi kati ya Tyson Fury dhidi ya Oleksandr Usyk huku nduguye Paul Pogba, Mathias Pogba akipokea kifungo cha miaka mitatu jela kwa kujaribu kumlaghai Paul Pogba pesa.
-
Kigali: Max Verstappen aongoza katika sherehe za Tuzo za FIA kwenye mkutano mkuu
14/12/2024 Duración: 23minTulikuandalia ni pamoja na yaliyozungumziwa kwenye mkutano mkuu wa shirikisho la mchezo wa kuendesha magari duniani, FIA nchini Rwanda, uchambuzi wa raundi ya tatu ya mechi za ligi ya mabingwa Afrika, Pape Thiaw ateuliwa kuwa kocha mpya wa Senegal, Afrika Kusini yashinda Kombe la Afrika mchezo wa pete, uchambuzi wa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya, Saudi Arabia ikithibitishwa kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2034
-
Hussein Mohammed ashinda kiti cha urais shirikisho la soka FKF nchini Kenya
07/12/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na uchaguzi wa shirikisho la soka nchini Kenya FKF, raundi ya pili ya klabu bingwa Afrika na raga ya wachezaji saba kila upande duniani, fainali za kombe la mataifa ya Afrika mchezo wa handboli kwa kina dada, debi la Rwanda, mechi za kufuzu ligi ya Afrika basketboli mwaka ujao, droo ya makundi michuano ya klabu bingwa duniani mwaka ujao nchini Marekani mwaka 2026.
-
Fahamu mchezo wa Tong IL Moo Do kuelekea mashindano ya Mombasa Open 2024
30/11/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na mahojiano ya moja kwa moja na washikadau wa mchezo wa Tong IL Moo Do ambao walitutembelea studioni. Mchezo huu unazidi kukua Afrika. Je, unachezwaje, nini umuhimu wake, umepiga hatua kiasi gani, maandalizi ya makala ya Mombasa Open ya mwaka huu yakoje? Pia tumeangazia Ligi ya Klabu bingwa Afrika, msimu mpya wa raga ya HSBC duniani na Kombe la Mataifa ya Afrika ya kina dada mchezo wa handboli ambayo ilianza wiki hii pamoja na uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya
-
CAF: Droo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada yakamilika
23/11/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa droo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada 2024, fainali ya klabu bingwa Afrika kwa kina dada, nini maana ya Tanzania na Uganda kuwakilisha CECAFA kwenye AFCON 2024, mechi za kufuzu ligi ya Afrika ya Basketboli na michuano ya kufuzu Mashindano ya Afrika ya Basketboli, ligi za ukanda na ulaya Pep Guardiola atia saini mkataba mpya klabuni Man City.
-
AFCON 2025: Uganda yafuzu fainali za mwaka kesho huku Kenya, Ghana zikitupwa nje
16/11/2024 Duración: 23minTuliyoyazungumzia ni pamoja na upekee wa klabu ya voliboli nchini Kenya ya Trailblazers, uchaguzi wa FKF nchini Kenya umeanza, mabadiliko ya makocha klabuni Yanga, timu ya taifa ya Kenya ya walemavu ya soka yamaliza nafasi ya nne Kombe la Dunia, uchambuzi wa michuano ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2025 na pigano la Jake Paul dhidi ya Mike Tyson
-
CAF: Ligi ya klabu bingwa barani Afrika 2024 kwa kina dada yaanza nchini Morocco
09/11/2024 Duración: 23minTumeangazia klabu ya Chaux Sport kutoka DRC kubanduliwa kwenye mechi za kufuzu Ligi ya Basketboli Afrika 2024, masaibu ya Yanga SC nchini Tanzania, uchaguzi wa FKF nchini Kenya, mashindano ya kuendesha baiskeli Afrika kwa kina dada nchini Burundi, kifo cha rais wa soka nchini Algeria, matokeo na uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya na fainali ya tenisi kwenye mashindano ya WTA