Jukwaa La Michezo

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 9:47:36
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali. 

Episodios

  • CAF: Niger, Sudan na Zambia zafuzu mashindano ya soka ya CHAN 2024

    28/12/2024 Duración: 23min

    Ikiwa Jumamosi ya mwisho ya mwaka 2024, tunakuuliza ni tukio gani au mashindano gani ya kispoti yalikufurahisha zaidi mwaka huu? Pamoja na hayo; tumeangazia kifo cha mchezaji nguli wa voliboli nchini Kenya Janet Wanja, Uganda yaibuka mabingwa wa CECAFA michuano ya kufuzu AFCON U17, raundi ya mwisho ya kufuzu michuano ya CHAN 2024, uchambuzi wa raundi ya 18 ya mechi za Ligi Kuu ya Soka nchini Uingereza. 

  • CHAN 2024: Rais Motsepe aridhishwa na maandalizi ya Kenya, Uganda na Tanzania

    21/12/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa ziara ya rais wa CAF Patrice Motsepe Afrika Mashariki kuukagua maandalizi ya CHAN 2024, tuzo za wanasoka bora Afrika na FIFA mwaka huu, pigano la ndondi kati ya Tyson Fury dhidi ya Oleksandr Usyk huku nduguye Paul Pogba, Mathias Pogba akipokea kifungo cha miaka mitatu jela kwa kujaribu kumlaghai Paul Pogba pesa.

  • Kigali: Max Verstappen aongoza katika sherehe za Tuzo za FIA kwenye mkutano mkuu

    14/12/2024 Duración: 23min

    Tulikuandalia ni pamoja na yaliyozungumziwa kwenye mkutano mkuu wa shirikisho la mchezo wa kuendesha magari duniani, FIA nchini Rwanda, uchambuzi wa raundi ya tatu ya mechi za ligi ya mabingwa Afrika, Pape Thiaw ateuliwa kuwa kocha mpya wa Senegal, Afrika Kusini yashinda Kombe la Afrika mchezo wa pete, uchambuzi wa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya, Saudi Arabia ikithibitishwa kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2034

  • Hussein Mohammed ashinda kiti cha urais shirikisho la soka FKF nchini Kenya

    07/12/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na uchaguzi wa shirikisho la soka nchini Kenya FKF, raundi ya pili ya klabu bingwa Afrika na raga ya wachezaji saba kila upande duniani, fainali za kombe la mataifa ya Afrika mchezo wa handboli kwa kina dada, debi la Rwanda, mechi za kufuzu ligi ya Afrika basketboli mwaka ujao, droo ya makundi michuano ya klabu bingwa duniani mwaka ujao nchini Marekani mwaka 2026.

página 2 de 2