Sinopsis
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Episodios
-
Mwaka mpya wa 2025 na matarajio ya ulimwengu kuhusu usalama amani na maendeleo
04/01/2025 Duración: 20minMakala hii imeangazia namna ambavyo nchi zetu zilivyoukaribisha mwaka wa 2025 kwa shamrashamra za kila aina huku wakisema kwaheri kwa mwaka 2024 ulioshuhudia michezo mikubwa zaidi ulimwenguni ya Olimpiki, vita ya Ukraine na kule Gaza, usalama mashariki mwa DRC, Sudan pamoja na kurejea madarakani kwa aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trump.
-
Polisi wa Kenya wasambaratisha maandamano, hotuba ya Tshisekedi bungeni DRC
14/12/2024 Duración: 20minMakala imeangazia namna ambavyo polisi nchini Kenya walivyotawanya maandamano ya wanaharakati waliopinga ukatili dhidi ya wanawake na mauaji nchini humo. Rais wa DRC Felix Tshisekedi alilihutubia taifa mbele y amabunge yote mawili, na kuonyesha kwamba Rwanda inatatiza usalama wa mashariki, siasa za Tanzania, Sudani, na Francois Bayrou ateuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Ufaransa pia hali nchini Israeli.
-
Ziara ya rais Joe Biden huko Angola, watano wahukumiwa kifo huko DRC
07/12/2024 Duración: 20minHabari kuu wiki hii ni pamoja na mkutano kati ya rais wa Marekani anayejiandaa kuondoka madarakani Joe Biden na viongozi wa Afrika huko Lobito Angola, mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini kuanza tena baada ya miezi minne, maafisa 20 wa Kenya waliopelekwa Haiti wajiuzulu, rais wa DRC Felix Tshisekedi kukutana na rais wa Rwanda Paul Kagame desemba 15, yaliyojiri Sudan uchaguzi nchini Ghana, na wabunge wa Ufaransa walivyoiangusha serikali ya Michel Barnier lakini pia kanisa kubwa la Notre Dame lafunguliwa jijini Paris Ufaransa, Israel yaendeleza mashambulizi Gaza
-
DRC:Rais Felix Tchisekedi awataka raia wa nchi yake kuunga mkono mabadiliko ya katiba
30/11/2024 Duración: 19minMiongoni mwa yale utakayoyasikia kwenye habari ni pamoja na Rais wa DRC, Felix Tschisekedi, kuwataka raia wa nchi yake kuunga mkono mabadiliko ya katiba, , Chama tawala cha CCM nchini Tanzania chaongoza kwa asilimia 99 ya kura.Zaidi ya watu 100 hawajulikani walipo baada ya ajali ya maporomoko ya Udongo nchini Uganda,pia Tutaangazia ziara yake Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, nchini Ufaransa, Raia wa Namibia wapiga kura, kisha kimataifa tutaangazia mkutano wa Mawaziri wa mambo ya nje kutoka muungano wa G7,uliofanyika mjini Roma Italia.