Sinopsis
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Episodios
-
Mfano wa Misri wa kupambana na Malaria unaweza kutumika na mataifa ya Afrika
13/05/2025 Duración: 09minMisri imepambana kwa karibu miaka 100 kabla kupata cheti cha WHO cha kufaulu kutokomeza Malaria Oktoba 2024 Katika mkakati ambao umetumia Misri kuangamiza Malaria ni udhibiti wa Mbu,ambapo serikali iliwekeza kwenye kupiga dawa kwenye maeneo yanayoweza kuwa makazi ya mbu .Ufuatiliaji na ubainishaji wa haraka umechangia pia pakubwa kuushinda ugonjwa wa Malaria ,mkakati ambao pia jamii ilibidi kushirikishwa.Kitengo cha afya ya umma kimekuwa kikifanya hamasisho kwa wanajamii kukumbatia mbinu za kuzuia mbu kwa kutumia vyandarua na pia kupata matibabu ya haraka mtu anapoonesha dalili za Malaria.
-
Mchango wa wanaveterinari ulivyo muhimu katika mapambano ya magonjwa ya milipuko
03/05/2025 Duración: 10minOngezeko la magonjwa ya milipuko linaibua swala la kwa nini watalaam wa wanyama hawahusishwi kikamilifu katika mifumo ya afya ya binadaam Mpango wa one Health Approach unaonadiwa kwa sasa kwa mataifa ,unahimiza kuipa kipau mbele afya ya wanyama ,ili kuchangia siha njema ,usalama wa chakula na maendeleo endelevu .
-
Kwa nini ni muhimu kuyachunguza maziwa unayotumia nyumbani kulinda afya yako
03/05/2025 Duración: 10minKumekuwa na malalamishi ya maziwa yaliyo kwenye soko kusababisha madhara ya kiafya Watalaam wa afya ,bodi inayosimamia bidhaa za maziwa nchini Kenya na wanavetirinari wanasema matatizo hayo huenda yanatokana na uzembe wakati wa uchakataji maziwa ,uhifadhi na pia wafanyabiashara wenye pupa.
-
Changamoto zinazowakumba watalaam wanaojikita kwenye tiba asilia nchini DRC
08/04/2025 Duración: 10minBaadhi ya changamoto zinazokumba sekta ya tiba asilia ni mwitiko na ukosefu wa sheria za kuisimamia katika nchi mbali mbali