Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 4:00:30
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.

Episodios

  • Mwali wa mwisho: Mkaa wa Briketi kama suluhu ya nishati jadidifu

    20/02/2025 Duración: 09min

    Mkaa wa Briketi hutengenezwa kutoka kwa vumbi la mkaa wa kawaida, taka za kilimo au mabaki ya mbao, na hutumiwa kimsingi kwa mapishi nyumbani, shuleni na hata katika makampuni. Mkaa huu una faida kwa kuwa unapunguza uchafuzi wa mazingira, kupunguza ukataji wa miti lakini pia huwaka kwa muda mrefu na kwa usawa zaidi kuliko mkaa wa kawaida, na kuufanya kuwa chaguo maarufu kwa kupikia.

  • Umuhimu wa matumizi ya madawa ya kiasili kunyunyuzia mimea shambani

    10/02/2025 Duración: 10min

    Makala haya yanazungumzia  jinsi Wakulima wengi nchini Kenya wanakumbatia mbinu mpya za kudhibiti wadudu waharibifu wa mimea kwa kutumia madawa ya kiasili badala ya kemikali za viwandani. Kutokana na madhara yanayotokana na matumizi ya dawa za kemikali,wakulima hawa sasa wanageukia madawa hayo asilia kuimarisha mazao na mazingira , Mimea kama vile ,pareto,kitunguu saumu,pilipili na hata mtunguja pori yaani sodom apple sasa inatumika kutengeneza madawa hayo.

  • Wakaaji wa mijini wanavyotumia Bustani ya Nyumbani kukabili mabadiliko ya tabia nchi

    03/02/2025 Duración: 09min

    Utunzaji wa bustani ya nyumbani, ni mbinu mpya ya kilimo inayolenga kutimiza malengo matatu kwa wakati mmoja: kuongeza mapato ya kilimo, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuimarisha ustahimilivu, halkadhalika kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi. Bustani ya Nyumbani, kwa kawaida huwa karibu na jikoni au pia kwenye roshani. Bustani hii ambayo mara nyingi hutumia mbolea asilia husaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu na pia kutunza udongo.Bustani hii hutumika kwa kilimo cha mboga, viungo vya upishi kama vitunguu, matunda, au mimea ya kitiba kwa matumizi.

  • Hatua ya Marekani kujiondoa kwa mkataba wa Paris kuathiri nchi maskini

    28/01/2025 Duración: 09min

    Rais Donald Trump kwa mara nyingine alitangaza Marekani kujiondoa kwenye Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, hatua ambayo imeibua mjadala wa kimataifa.  Tangazo hilo lilikuja huku ulimwengu ukishuhudia viwango vya joto vinavyovunja rekodi na majanga yanayozidi kuwa makali yanayohusiana na hali ya hewa.Lakini wadadisi wa mambo na viongozi wengine wa ulimwengu wanatazamaje hatua yake Trump? Bonyeza usikilize zaidi.

página 2 de 2