Sinopsis
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
Episodios
-
Kilimo na teknolojia ya Akili Mnemba Afrika
23/04/2025 Duración: 10minKatika juhudi za kuimarisha ubunifu na ushindani wa kilimo biashara barani Afrika, Kenya kwa kushirikiana na Ufaransa zimeanzisha mpango wa mafunzo ya matumizi ya teknolojia kwa wakulima wanawake, yakiangazia Akili Mnemba (AI) kuongeza thamani ya mazao, mpango umefikia zaidi ya vikundi na mashirika 1200 ya wanawake wakulima na kuwawezesha kutumia teknolojia za kisasa kuongeza ubora, usindikaji na masoko.
-
Sehemu II: Madhara ya ushuru wa Trump kwa bara la Afrika na biashara ya dunia
16/04/2025 Duración: 09minMsikilizaji kwa majuma kadhaa sasa, kumekuwa na mjadala duniani kote kufuatia uamuzi wa rais wa Marekani, Donald Trump, kutangaza ushuru wa bidhaa zinazoingia kwenye taifa hilo, mataifa ya Afrika yakiwa miongoni mwa waathirika, baadhi wakiwekewa ushuru wa hadi asilimia 50. Hata hivyo juma lililopita, rais Trump alitangaza kusitisha kwa muda wa siku 90 utekelezwaji wa ushuru kwa baadhi ya mataifa isipokuwa Uchina, ambayo imewekewa ushuru wa zaidi ya asilimia 125.Katika sehemu hii ya pili ya makala ya wiki hii, tumezungumza na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara.
-
Sehemu I: Madhara ya ushuru wa Trump kwa bara la Afrika na biashara ya dunia
09/04/2025 Duración: 10minKwa majuma kadhaa, mijadala mikali duniani kote kufuatia uamuzi wa rais wa Marekani, Donald Trump, kutangaza ushuru zaidi wa bidhaa zinazoingia kwenye taifa hilo, mataifa ya Afrika yakiwa miongoni mwa waathirika, baadhi wakiwekewa ushuru wa hadi asilimia 50. Katika makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunadadavua na wataalamu athari za ushuru wa Trump kwa nchi za Afrika na biashara ya dunia kiujumla. Tutakuwa na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.