Sinopsis
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
Episodios
-
Utamaduni wa watu wa makabila ya wahangaza na wamakonde kutoka nchini Tanzania
22/09/2024 Duración: 20minKatika makala haya, mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na Amua Rushita kutoka Mkoa wa Mtwara pamoja na Hilali Alexanda Ruhundwa kutoka Mkoa wa Kagera Wilaya ya Ngara nchini Tanzania kuzungumzia utamaduni wa ndoa kulingana na makabila hayo mawili. Kumbuka pia nawe unaweza kushiriki moja kwa moja studio au kwa njia ya simu. Wasiliana na mtangazaji wako asiependa makuu kufahamu zaidi.
-
Toleo la 11 la Bourse Ghislaine Dupont na Claude Verlon kutolewa huko Benin
26/08/2024 Duración: 19minRFI inaandaa toleo la kumi na moja la Bourse Ghislaine Dupont na Claude Verlon, kwa heshima kwa waandishi wake wawili waliouawa kaskazini mwa Mali Novemba 2, 2013. Bourse hii, ambayo huwafunza waandishi wa habari vijana kumi wa redio na mafundi vijana kumi wa kuripoti kila mwaka, iko wazi. kwa wagombea kutoka nchi zote za Afrika zinazozungumza Kifaransa. Mafunzo hayo yatafanyika Cotonou. Maombi yamefunguliwa hadi Jumapili Agosti 25 saa sita usiku saa za Paris.
-
Changu Chako Chako Changu: Utamaduni wa mahari kwa baadhi ya makabila barani Afrika
26/08/2024 Duración: 19minMakala haya yanaangazia kuhusu gharama ya sherehe za harusi katika karne hii, hususan ukusanyaji wa michango kwa ajili ya kufanaikisha sherehe.