Sinopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodios
-
Kutimiza azimio la watu wa jamii za asili ni jukumu la mataifa yote duniani - Adam Ole Mwarabu
08/05/2025 Duración: 06minJukwaa la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa jamii za asili limekunja jamvi mwishoni mwa wiki iliyopita hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na kandoni mwa jukwaa hilo Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa washiriki kiongozi wa kijamii kutoka Jamii ya wafugaji ya Wamaasai mkoani Morogoro Mashariki mwa Tanzania Adam Kulet Ole Mwarabu, wamejadili mengi lakini Ole Mwarabu anaanza kwa kukumbusha alichokibeba kwenye jukwaa la mwaka jana kinavyotekelezwa nchini mwake.
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "DALALI”
08/05/2025 Duración: 45sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "DALALI”
-
08 MEI 2025
08/05/2025 Duración: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa ambayo Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na kiongozi wa kijamii kutoka Jamii ya wafugaji ya Wamaasai mkoani Morogoro nchini Mashariki mwa Tanzania Adam Kulet Ole Mwarabu.Wiki kumi baada ya kuanza kwa mzingiro kamili wa Israel dhidi ya wakazi wa Gaza, zaidi ya robo tatu ya kaya katika eneo la Palestina kuna uhaba mkubwa wa huduma ya maji, huku hali ya usafi ikizidi kuwa mbaya, yameonya leo mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu athari za "uhaba huo wa maji kwa kuzingatia kuwa msimu wa joto unakaribia.”Ripoti kutoka Sudan zikidai kwamba juzi jumatano kulikuwa na jaribio la mashambulizi mapya ya ndege zisizo na rubani dhidi ya kitovu muhimu cha misaada nchini humo juzi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia tamko alilolitoa jana jioni kwa saa za New York, Marekani, ameongeza nguvu yake katika kutoa wito unaozidi kuwa wa muhimu kuhamasisha kuanzishwa kwa mazungumzo ya amani ya kweli.Kufuati
-
Operesheni za kijeshi Jammu na Kashmir hazina tija – Guterres
07/05/2025 Duración: 02minHuko barani Asia majirani wawili India na Pakistani wameendelea kuoneshana mvutano kati yao kwenye eneo la Jammu na Kashmiri tangu tarehe 22 mwezi uliopita wa Aprili baada ya shambulizi huko Pahalgam. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kama anavyoelezea Assumpta Massoi.
-
07 MEI 2025
07/05/2025 Duración: 10minHii leo jaridani tunaangazia mvutano unaoendelea barani Asia kati ya majirani wawili India na Pakistani, na msaada wa mguu bandia uliowezesha mtototo nchini Kenya kwenda shule. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani tunakwenda katika ukanda wa Gaza.Huko barani Asia majirani wawili India na Pakistani wameendelea kuoneshana mvutano kati yao kwenye eneo la Jammu na Kashmiri tangu tarehe 22 mwezi uliopita wa Aprili baada ya shambulizi huko Pahalgam. Katibu Mkuu ametoa wito kwa mara nyingine tena.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau wameleta neema kwa watoto wanaoishi na ulemavu katika Kaunti ya Kisumu Magharibi mwa Kenya baada ya kuwapa msaada wa vifaa ikiwemo viti mwendo na viungo bandia kupitia mradi wa ubunifu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, msaada uliobadili maisha yao.Makala katika wiki ya chanjo duniani, iliyotamatishwa tarehe 30 wiki iliyopita, mtaa wa Butiama, ulioko Mtoni Kijichi katika wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania ulishu
-
Wazazi pelekeni watoto wenu kupata chanjo dhidi ya maradhi - Bi. Halfani
07/05/2025 Duración: 03minKatika Wiki ya Chanjo duniani, iliyotamatishwa tarehe 30 wiki iliyopita, mtaa wa Butiama, ulioko Mtoni Kijichi katika wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania ulishuhudia wazazi na walezi wakijitokeza kuwapatia watoto wao chanjo muhimu za kuwalinda dhidi ya maradhi hatari. Miongoni mwao ni Hija Halfani ambaye alimpeleka mtoto wake mwenye umri wa siku 42 kupata chanjo yake ya kwanza. Je, ni mafanikio gani yamepatikana na kwa nini chanjo hizi ni muhimu? Ungana na Sharon Jebichii kwa makala hii iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania.
-
Evelyn Atieno: Asante UNICEF kwa kubadili Maisha ya mwanangu Fidel
07/05/2025 Duración: 02minShirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau wameleta neema kwa watoto wanaoishi na ulemavu katika Kaunti ya Kisumu Magharibi mwa Kenya baada ya kuwapa msaada wa vifaa ikiwemo viti mwendo na viungo bandia kupitia mradi wa ubunifu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, msaada uliobadili maisha yao. Flora Nducha amefuatilia tabasamu la mama ambaye mwanye amenufaika na kiungo bandia ungana naye kwa tarifa zaidi
-
06 MEI 2025
06/05/2025 Duración: 12minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha hapa makao makuu ambako Idhaa hii Dokta Willis Ochieng kutoka Kenya aliyehudhuria ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya kilimo na maendeleo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari, na mashinani tunakwenda Ghana.Ukuaji wa maendeleo ya binadamu – yanayopimwa kwa uhuru na ustawi wa watu – umeendelea kuwa wa kasi ndogo tangu mshtuko mkubwa wa janga la COVID-19 lakini kuna matumaini makubwa kwamba Akili Mnemba au AI, ikiwa itatumika kwa njia sahihi, inaweza kuwa chombo chenye nguvu cha kuboresha maisha ya mamilioni ya watu. Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya kila mwaka ya Maendeleo ya Binadamu iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP.Kulengwa kwa hospitali ya Médecins Sans Frontières nchini Sudan Kusini kunaweza kuwa uhalifu wa kivita imeeleza leo Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu Sudan Kusini kufuatia mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa dhidi ya
-
VoTAN sio tu mtandao wa kidijitali kusaidia manusura wa ugaidi bali pia ni familia - Manusura
05/05/2025 Duración: 05minHatimaye kilio cha manusura wa ugaidi duniani cha kuwa na Mtandao wa Mashirika yao ili kuweza kupaza zaidi sauti zao kwa ajili ya sio tu kusaidiwa bali pia kuepusha matukio kama hayo, kimepata jawabu baada ya Mtandao huo au VoTAN kuzinduliwa kwenye Umoja wa Mataifa. Kwa msaada wa kifedha kutoka Hispania, Iraq na nchi nyingine wanachama, mtandao huu ulio chini ya Programu ya kusaidia manusura wa ugaidi kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kukabilana na Ugaidi, UNOCT, unatarajiwa kuziba mapengo ya msaada na kuinua ushuhuda wa manusuta kutoka maeneo yaliyopuuzwa duniani. Assumpta Massoi amefuatilia uzinduzi huo na kuandaa makala hii.
-
MONUSCO yapatia wanawake wakimbizi DRC mafunzo ya ushoni
05/05/2025 Duración: 02minWanawake 125 katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kigonze, karibu na Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako ghasia huripokiwa mara kwa mara, sasa wana matumaini mapya ya kujikwamua kiuchumi baada ya kujiunga na mradi wa mafunzo ya kushona nguo unaofadhiliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo (MONUSCO). Sharon Jebichii na taarifa kamili.
-
05 MEI 2025
05/05/2025 Duración: 10minHii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya wakunga na kazi zao muhumi, na mafunzo ya jerahani kwa wakimbizi wa ndani nchini DRC. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakwenda Gaza.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wakunga, tunakwenda nchini Tanzania kummulika mkunga ambaye alinusuru maisha ya wajawazito wawili wakati wa mafuriko makubwa ya Novemba 2023 wilayani Hanang, mkoani Manyara, kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ikiwa ni ushuhuda wa majukumu mazito yanayokumba wakunga.Wanawake 125 katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kigonze, karibu na Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako ghasia huripokiwa mara kwa mara, sasa wana matumaini mapya ya kujikwamua kiuchumi baada ya kujiunga na mradi wa mafunzo ya kushona nguo unaofadhiliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo (MONUSCO).Makala Assumpta Massoi anamulika uzinduzi wa mtandao wa Mashirika ya Manusura wa Ugaidi duniani, VoTAN&n
-
Mkunga nchini Tanzania atoa wito wa uwekezaji kwenye fani hiyo
05/05/2025 Duración: 02minIkiwa leo ni siku ya kimataifa ya wakunga, tunakwenda nchini Tanzania kummulika mkunga ambaye alinusuru maisha ya wajawazito wawili wakati wa mafuriko makubwa ya Novemba 2023 wilayani Hanang, mkoani Manyara, kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ikiwa ni ushuhuda wa majukumu mazito yanayokumba wakunga. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
-
Bila mafunzo watu tutakuwa watumiaji tu wa AI na sio wanaufaika: Hassan Mhelela
02/05/2025 Duración: 05minKatika kuelekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani itakayoadhimishwa Jumamosi Mei 3 ambayo mwaka huu imebeba maudhui yanayoangazia athari za Akili Mnemba au AI katika uhuru wa habari na vyombo vya habari tunazungumza na mmoja wa wanahabari wa siku nyingi ili kufahamu AI inavyoleta mabadiliko katika tasnia ya habari na vyombo vya habari hususan Afrika Mashariki ambako pia pengo la kidijitali ni kubwa. Ungana na Flora Nducha kwa undani zaidi katika makala hii.
-
Akili mnemba au AI ni sawa na upanga wenye makali pande mbili - Guterres
02/05/2025 Duración: 01minKuelekea siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari Mei 3, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema waandishi wa habari wanakabiliwa na hatari kila uchao huku teknolojia mpya ya akili mnemba au AI ingawa licha ya manufaa nayo pia inaibua hatari mpya kwenye uhuru wa kujieleza. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.
-
02 MEI 2025
02/05/2025 Duración: 11minHii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari Mei 3 tukikuletea ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu umuhimu wake. Pia tunamulika hali ya msaada wa kibinadamu nchini Sudan.Kuelekea siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari Mei 3, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema waandishi wa habari wanakabiliwa na hatari kila uchao huku teknolojia mpya ya akili mnemba au AI ingawa licha ya manufaa nayo pia inaibua hatari mpya kwenye uhuru wa kujieleza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, (WFP) tayari limeanza usambazaji wa chakula katika maeneo mbalimbali ya Sudan ambako watu wanakabiliwa na jaa huku wengine wakilazimika kuhama kambi moja hadi nyingine.Makala inamulika siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani itakayoadhimishwa kesho Jumamosi Mei 3 ambayo mwaka huu ikijikita na athari za Akili Mnemba au AI katika uhuru wa habari za vyombo vya habari. Ili kufahamu AI inavyoleta mabadiliko katika vyombo vya habari hususan Afrika Mashariki ambako pia
-
WFP yaongeza usambazaji wa chakula nchini Sudan japo hali bado tete
02/05/2025 Duración: 01minShirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, (WFP) tayari limeanza usambazaji wa chakula katika maeneo mbalimbali ya Sudan ambako watu wanakabiliwa na jaa huku wengine wakilazimika kuhama kambi moja hadi nyingine. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
-
Maoni kutoka washiriki kutoka maeneo mbalimbali waliohudhuria mkutano wa jamii za asili UNPFII
30/04/2025 Duración: 03minHapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa 24 wa Jukwaa la Kudumu la Watu wa jamii za asili (UNPFII) linaendelea kujadili utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili na kubaini mbinu bora za kushughulikia changamoto zinazowakabili, ukileta pamoja washiriki kutoka maeneo mbalimbali kote duniani. Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa walipata fursa ya kuzungumza na baadhi yao.
-
UNESCO: Jazz ni daraja la kudumisha amani, uhuru na mshikamano
30/04/2025 Duración: 04minLeo tarehe 30 Aprili dunia nzima inaburudika kwa pamoja kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Jazz, Kuanzia New Orleans hadi Nairobi, Tokyo hadi Tunis, miji inawasha taa majukwaani na mioyoni kusherehekea midundo yenye ladha ya kale, ya kisasa na yenye mvuto wa kipekee. Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO linasema Jazz ni zaidi ya muziki, ni daraja la kuunganisha watu na kuleta utangamano. Flora Nducha anatupasha zaidi katika makala hii
-
Ripoti kuhusu Mpox yazitaja nchi 11 za Afrika, Ulaya, China na Amerika nao wamo
30/04/2025 Duración: 02minMaambukizi ya ugonjwa wa mpox kutokana na aina ya virusi vya monkeypox clade Ib /ˈmʌŋ.ki.pɑks kleɪd one bee/ (MPXV) yanaendelea kuripotiwa hasa barani Afrika, ambapo mataifa kumi na moja yameripoti maambukizi ya ndani ya jamii katika kipindi cha wiki sita zilizopita. Hiyo kwa mujibu wa ripoti 51 ya Shrika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO kuhusu hali ya mlipuko wa mpox katika nchi mbalimbali duniani. Anold Kayanda amefuatilia ripoti hiyo na anatufafanulia kwa ufupi.
-
30 APRILI 2025
30/04/2025 Duración: 11minHii leo jaridani tunaangazia ugonjwa wa mpox, na walinda amabini wa Umoja wa Mataifa nchini DR Congo. Makala inamuulika siku siku ya kimataifa ya muziki wa Jazz namashinani tunasalia hapa makao maku kusikia ujumbe wa mwakilishi wa shirika la watu wa jamii za Asili.Maambukizi ya ugonjwa wa mpox kutokana na aina ya virusi vya monkeypox clade Ib /ˈmʌŋ.ki.pɑks kleɪd one bee/ (MPXV) yanaendelea kuripotiwa hasa barani Afrika, ambapo mataifa kumi na moja yameripoti maambukizi ya ndani ya jamii katika kipindi cha wiki sita zilizopita. Hiyo kwa mujibu wa ripoti 51 ya Shrika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO kuhusu hali ya mlipuko wa mpox katika nchi mbalimbali duniani.Huko Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani kutoka Bangladesh na Indonesia, wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wamepatiwa medali kwa mchango wao wa ulinzi wa raia, moja ya jukumu kubwa la ujumbe huo..Makala ikiwa leo ni siku ya kimat