Sinopsis
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episodios
-
Rais wa DRC, Felix Tschsekedi, atangaza kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa
24/02/2025 Duración: 10minKaribu kwenye kipindi cha leo ambapo tunaangazia tangazo la Rais wa DRC, Felix Tschsekedi, kuwa ataunda Serikali ya umoja wa kitaifa, hatua inayokuja wakati huu akiwa katika shinikizo kutoka ndani na nje ya nchi yake, kuhusu namna alivyoshughulikia mzozo wa mashariki mwa nchi yake, wakati huu waasi wa M23 wakichukua miji zaidi.
-
Mada Huru: Maoni kuhusu habari kuu wiki hii na matukio katika maeneo mbalimbali
21/02/2025 Duración: 09minIkiwa ni siku ya Ijumaa, ni wakati wa mada huru, yaani tunampatia mskilizaji nafasi kuchangia habari kuu ambazo tumekuwa nazo wiki hii hapa RFI Kiswahili au kutueleza jambo ambalo limetokea nchini mwake juma hili. Leo pia msikilizaji ni siku ya lugha mama, ningependa sana nikusalimie kwa lugha yako mama lakini ningependa kusikia kutoka kwako kwanza. Jambo!
-
Maoni: Marekani yaanza mazungumzo na Urusi ya kusitisha vita nchini Ukraine.
21/02/2025 Duración: 09minHaya ni makala ya Habari Rafiki tukiangazia maoni ya waskilizaji wa RFI Kiswahili kuhusu mada kwamba, Marekani imeanza mazungumzo na Urusi, lengo likiwa kupata mkataba wa kusitisha vita nchini Ukraine. Ukraine ambayo haijashirikishwa kwenye mchakato huo inasema haitakubali mkataba wowote bila kuhusishwa.Tumemuuliza msikilizaji je, Marekani inaweza kumaliza vita vya Ukraine? Na anafikiri ni kwanini Marekani haijaishirikisha Ukraine na mataifa ya Ulaya kwenye harakati hizi?
-
Wanamgambo wa RSF waandaa mkutano wa kuunda serikali mbadala Nairobi
19/02/2025 Duración: 10minWanamgambo wa RSF wanaopigana na jeshi nchini Sudan na washirika wake wakiwemo wanasiasa wapo jijini Nairobi nchini Kenya, wanakojadiliana kuhusu uundwaji wa serikali mbadala wakati huu inapoendelea na vita.Unazungumzia vipi harakati hizi za RSF ?Unafikiri ni kwanini Kenya imewaruhusu wanamgambo hao kukutana katika nchi yake ?
-
Kikao cha usalama wa DRC na Sudan chakamilika Ethiopia bila suluhu
17/02/2025 Duración: 10minMakala ya leo yanaangazia Kikao cha viongozi wa Afrika, kilichotamatika rasmi mwishoni mwa juma lililopita nchini Ethiopia, mzozo wa DRC na Sudan ukigubika mijadala yao.Hata hivyo vikao hivyo vimekamilika bila suluhu ya mizozo ya nchi zote mbili, ambapo vyongozi waliishia kwa kutoa wito wa kusitisha mapigano. tulimuuliza msikilizaji iwapo anaridhika na matokeo ya kikao hicho na anadhani nini cha zaidi viongozi hawa wangefanya kukomesha mizozo barani Afrika
-
Mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Afrika kuzingatia usalama wa DRC
13/02/2025 Duración: 10minMkutano wa kila mwaka wa viongozi wa Afrika umeanza rasmi jijini Addis Ababa, #Ethiopia ambapo maswala muhimu ikiwemo usalama mashariki mwa #DRC, mapinduzi ya kijeshi na vita dhidi ya makundi ya kijihadi yakitarajiwa kugubika mkutano huu.Tulimuuliza mskilizaji natarajia nini kipya kutoka kwa viongozi wa AU? na iwapo anafikiri viongozi wameshindwa kumaliza changamoto za bara hili..
-
Kauli ya rais Donald Trump kuhamisha wapalestina yapingwa vikali
12/02/2025 Duración: 10minKwenye kipindi cha leo tunaangazia kauli tata ya Rais Donald #trump, kuhusu mzozo wa #Gaza, safari hii akitishia kuvunjika kwa mkataba wa usitishaji mapigano, ikiwa Hamas haitawaachia mateka wote ifikapo Jumamosi ya wiki hii.Juma lililopita alidai kuwa nchi yake itachukua udhibiti wa Gaza na kuwahamisha Wapalestina.Tulimuuliza mskilizaji anazungumziaje kauli hiyo ya Trump and je huenda zikachochea mzozo zaidi kati ya #Israel na Hamas?
-
Hatua ya Kenya kuondoa mahojiano kwa waomba vitambulisho yaibua hisia mseto
11/02/2025 Duración: 09minMakala haya yanaangazia hatua ya Serikali ya kenya kusema hakutakuwa na haja ya mahojiano kwa waomba vitambulisho toka katika maeneo ya mpakani, uamuzi ambao umeibua mjadala kuhusu masuala ya usalama.Tulimuuliza msikilizaji anazungumziaje hatua hiyo ya Kenya vile vile nchini mwake hali ikoje
-
Kauli ya mkutano wa SADC na EAC kuhusu amani nchini DRC waibua maoni mseto
10/02/2025 Duración: 09minkwenye makala ya leo tunaangazia hatua ya wakuu wa nchi za #SADC na EAC kutaka kusitishwa mapigano maramoja ,na kutaka kuondoka kwa vikosi vya kigeni mashariki mwa #DRC, pamoja na Serikali ya Kinshasa kuzungumza moja kwa moja na waasi wa #M23 ambapo wito huo umepokelewa kwa hisia mseto na raia wa ukanda.
-
Kila siku ya Ijumaa huwa tunaangazia mada huru kwenye makala habari rafiki
31/01/2025 Duración: 10minKila siku ya ijumaa ni mada huru ambapo Tunampa nafasi msikilizaji kujadili suala lolote ambalo limetokea nchini mwake wiki hii au kile ambacho amekisikiliza kwenye habari zetu juma hili.
-
Changamoto za upatikanaji wa Nishati ya Uhakika barani Afrika
30/01/2025 Duración: 09minWakuu wa nchi za Afrika walikutana juma hili nchini Tanzania ambapo walijadiliana kuhusu changamoto za upatikanaji wa Nishati ya Uhakika katika mataifa hayo.Licha ya rasilimali za bara la Afrika bado hakuna nishati ya uhakika na endelevu? Bonyeza uskilize maoni mbalimbali.
-
Athari za Donald Trump kusitisha misaada kwa Afrika na njia mbadala kujitegemea
30/01/2025 Duración: 10minUamuzi wa Rais wa Marekani #DonaldTrump, kuagiza kusitishwa kwa muda utowaji wa misaada yote ya kigeni umeibua mjadala na sintofahamu hasa kwa nchi za Afrika, ambazo sekta muhimu ikiwemo afya zinategemea msaada wa Marekani.Tulimuuliwa msikilizaji anazungumziaje hatua hii ya Marekani na Nchi za Afrika zifanye nini kuacha kutegemea misaada ya nchi za Kigeni?
-
Swali: Je viongozi wa Afrika wanaweza kutatua migogoro inayokumba bara hilo
29/01/2025 Duración: 09minMizozo inayosibu ukanda wa Afrika ya Mashariki inaendelea kuongezeka, ikiwemo Sudan Kusini na sasa DRC. Viongozi wa Afrika wanasisitiza matatizo ya Afrika sharti kutatuliwa kwa suluhu kutoka Afrika. Je hili linawezekana?
-
Wito wa mataifa ya Afrika kutafuta suluhu kwa matatizo ya Afrika
29/01/2025 Duración: 06minUkanda wa Afrika unazidi kushuhudia ongezeko la migogoro huku viongozi wakisisitiza Afrika ina majibu ya mizozo hiyo
-
Nani wa kulaumiwa kuhusu vita vinavyoendelea mashariki mwa DRC
23/01/2025 Duración: 10minMapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa serikali ya DRC yanayoendelea na sasa yamefika jimboni Kivu Kusini,Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya kibinadamu OCHA ikisema maelfu ya watu wameendelea kukimbia makaazi yao.Kwenye makala haya tumemuuliza msikilizaji nani wa kulaumiwa kuhusu vita hivi vinavyoendelea? na anafikiri ni kwanini imekuwa vigumu kupata suluhu?
-
Visa vya uchimbaji madini haramu vinazidi kuongezeka barani Afrika
22/01/2025 Duración: 09minVisa vya uchimbaji wa madini haramu vimeongezeka katika nchi mbalimbali barani Afrika .Afrika Kusini ikiwa mfano wa nchi hizo ambayo imeshuhudia miili ya wachimba midogo zaidi ya 70 ikipatikana katika mgodi wa dhahabu usiokuwa rasmi.Kwenye kipindi cha leo tumemuuliza msikilizaji anafkiri nchi za Afrika zimeshindwa kudhibiti uchimbaji haramu wa madini ? na nini kinaweza kufanyika kuzuia uchimbaji huo haramu ?
-
Dunia itarajie nini kutoka kwa uongozi wa Rais wa Marekani Donald Trump
21/01/2025 Duración: 09minKwenye kipindi cha leo tunaangazia kurejea afisini kwa rais wa Marekani Donald Trump baada ya kuapishwa kama rais na kuahidi nchi mpya.Tumemuuliza msikilizaji dunia itarajie nini kutoka kwa uongozi Wake na je Waafrika wana matumaini gani kuhusu kuongozi wake Trumpµ?
-
Wataalamu wa afya kutoka jumuia ya EAC wakutana Mombasa pwani ya Kenya
15/01/2025 Duración: 10minMakala ya habari rafiki imewashirikisha wasikilizaji kutoka kila kona ambapo wasikilizaji wametoa maoni yao kuhusu namna ambavyo wataalamu wa afya kutoka nchi za jumuia ya Afrika Mashariki walivyojadiliana kuhusu utaratibu wa kupata vibali kwenye nchi hizo bila ya kusumbuliwa. Ungana na Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi.
-
Kila siku ya Ijumaa kwenye makala Habari Rafiki ni Mada Huru
03/01/2025 Duración: 10minKila siku ya Ijumaa ni Mada huru ambapo tunakupa nafasi msikilizaji kuchangia suala lolote ambalo limetokea nchini mwake au kile ambacho amekisikia katika matangazo yetu ya wiki hii.
-
Viongozi wa Afrika mashariki watoa wito wa amani kwenye hotuba ya mwaka mpya
02/01/2025 Duración: 10minKatika salamu zao za mwaka mpya, viongozi karibu wote wa ukanda wa Afrika Mashariki, wametoa wito wa umoja na amani, huku kwa mataifa yenye utovu wa usalama, viongozi wakiahidi kirejesha utulivu.Tulimuuliza mskilizaji iwapo kiongozi wa nchi yake atabadili mambo mwaka huu wa 2025