Sinopsis
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episodios
-
Leo ikiwa ni siku ya ijumaa tarehe 08 08 2025 huwa ni mada huru .
08/08/2025 Duración: 10minLeo ni siku ya mada huru. Tunampa nafasi mskilizaji kuchangia suala lolote ambalo limejiri nchini mwake wiki hii,na pia anaweza kuzungumzia kile ambacho amekisikia katika matangazo yetu ya juma hili.
-
Hatua ya wanasiasa kuhama hama vyama baada ya kukosa kufaulu kwenye uteuzi
07/08/2025 Duración: 10minmada ya leo ni kuhusu Nchini Tanzania ambapo baadhi ya wanasiasa wa CCM ambao hawakufaulu katika uteuzi wa chama, wameanza kuhamia vyama vingine ili kugombea viti mbalimbali kwenye uchaguzi wa oktoba mwaka huu.Hali hii imekuwa ikishuhudiwa pia katika mataifa mbalimbali barani Afrika. Tunamuuliza msikilizaji anaizungumziaje hatua hii ya hama hama kisiasa,na hali hii inashuhudiwa nchini mwake,,
-
Majadiliano ya Geneva kuhusu hatua za kukabiliana na matumizi ya plastiki
06/08/2025 Duración: 10minWawakilishi kutoka kote duniani wanakutana, wako Geneva, kujadili hatua za mwisho za kukabiliana na matumizi ya bidhaa za plastiki ambazo zimeendelea kuharibu mazingira.Tumemuuliza msikilizani ni njia zipi mbadala zitumike badala ya bidhaa za plastiki na anafikiri ni kwa nini nchi hazitaki kuachana na matumizi ya mifuko ya Plastiki.
-