Sinopsis
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episodios
-
Tishio la kuzuka mzozo mpya kati ya Eritrea na Ethiopia kuhusu eneo la bahari
22/07/2025 Duración: 09minRais wa Eritrea Isaias Afwerki ameionya Ethiopia dhidi ya kuzuka tena kwa mzozo kwa kulazimisha kutumia eneo lake ya Bahari.
-
Afrika yaendelea kuathirika kufuatia hatua ya Marekani kusitisha misaada
21/07/2025 Duración: 10minNchini Zimbabwe wataalam wanasema wagonjwa wa Malaria wanaongezeka kwa kasi tangu Marekani kupitia shirika lake la USAID kukatisha misaada yake kwa nchi hiyo na bara la Afrika
-
Kenya yaondoa ulazima wa viza kwa mataifa ya Afrika isipokuwa Somalia na Libya
18/07/2025 Duración: 10min -
-
Marais wa Afrika kusalia madarakani kwa muda mrefu hata umri ukiwa umeenda
15/07/2025 Duración: 09min -
-
Kila Ijuma unapata nafasi kuchangia chochote ndani ya rfi Kiswahili
15/07/2025 Duración: 09minKila Ijumaa rfi kiswahili inakupa nafasi ya kuchangia mada yoyote ile kwenye makala haya. Skiza maoni ya waskilizaji.
-
Kenya : Maandamano yatumika kupora mali
15/07/2025 Duración: 09minMaandamano nchini Kenya na mataifa mengine ya Afrika yamekumbwa na mauaji na uporaji huku mali za watu zikiharibiwa. Je, unafikiri ni sahihi kwa waandamanaji kupora na kuharibu mali za watu? Nini vyombo vya usalama vinapaswa kufanya kuzuia uharibifu? Haya hapa baadhi ya maoni yako.
-
Viongozi wa Afrika wanatuhumiwa kuahidi mengi wakati wa kampeni na kutotimiza
14/07/2025 Duración: 09min -
Kenya: Mahakama ya juu yasema mwana haramu si haramu
09/07/2025 Duración: 09minKatika makala haya tujadili hatua ya mahakama ya juu zaidi nchini Kenya, kuagiza kwamba mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa kwenye dini ya kiislamu ana haki ya kumiliki mali ya babake kama watoto wengine waliozailiwa ndani ya ndoa, hatua inayoenda kinyume kabisa na tamaduni za dini hiyo. Unazungumziaje uamuzi huu wa mahakama nchini Kenya ? Haya hapa baadhi ya maoni yako.
-
Côte d'Ivoire : Kurejeshewa ngoma maalum kutoka Ufaransa
08/07/2025 Duración: 09minKaika makala haya tunajadili hatua ya bunge nchini Ufaransa kupiga kura na kupitisha mswada wa kurudishwa nchini Ivory Coast ngoma maalum inayozungumza iliyochukuliwa katika nchi hiyo ya Afrika kutoka kabila la Ebrie wakati wa ukoloni mwaka 1916. Je umefika wakati kwa koloni za zamani za Bara la Afrika kurejesha vyombo walivyopora ? Ndilo swali tumekuuliza . Haya hapa maoni yako.
-
Siku ya lugha ya kiswahili duniani makala maalum
07/07/2025 Duración: 10minSiku ya kiswahili duniani, ambayo imekuwa ikiadhimishwa tangu mwaka 2022. Maadhimisho ya mwaka huu imefanyika jijini Kigali nchini Rwanda, ambako mamia ya wataalam na wapenzi wa Kiswahili wamekutana kwa siku mbili kujadiliana kuhusu nafasi na umuhimu wa lugha ya Kiswahili kwa raia wa nchi zote za Jumuiya. Kauli mbiu ni kusherehekea lugha ya Umoja, utambulisho na mchango wake kwa dunia.RFI kiswahili imeshirikiana na taasisi ya mafunzo ya biashara na ufundi stadi, NIBS ya jijini Nairobi, kuandaa makala maalum ya Habari RAFIKI na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ameongoza makala hii
-
-
Watu karibu 500 wakamatwa nchini Kenya kufuatia maandamano ya Juni 25 2025
02/07/2025 Duración: 10minWanatuhumiwa kwa mauaji, ugaidi, ubakaji na makosa mengine. Wanaharakati wa haki za binadamu, wanasema, wanawake 14 walibakwa wakati wa maandamano hayo.
-
-
Mkataba kati ya DRC na Rwanda ya kuleta amani yakudumu mashariki mwa DRC
30/06/2025 Duración: 09minUmoja wa Afrika umekaribisha makubaliano yaliyotiwa saini mwishoni mwa juma lililopita kati ya Rwanda na DRC, hatua ambayo itashuhudia unyang'anyaji wa silaha na kuondolewa kwa mamluki wa kigeni mashariki mwa Congo.
-
-
Hatua ya bunge la Uingereza kuruhusu huduma ya kusaidiwa kufa
26/06/2025 Duración: 09minBunge la Uingereza hivi majuzi liliidhinisha mswada wa huduma ya kusaidiwa kufa
-
Maandamano ya kumbukizi ya kuwauwa kwa vijana zaidi ya 60 mwaka jana
25/06/2025 Duración: 10minWaandamanaji wakabiliana na polisi siku nzima wakati ya maandamano ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha wakati wa maandamano ya mwaka jana ya Gen Z
-
Zambia :Rais Hakainde Hichilema asisitiza serikali kufanya mazizi ya Edgar Lungu
24/06/2025 Duración: 10minRais wa Zambia Hakainde Hichilema ameendelea kusisitiza kufanya mazishi ya kitaifa kwa mtagulizi wake Edgar Lungu Licha ya mzozo uliopo baina yake na familia juu ya utekelezwaji ya matakwa ya marehemu ya kukataa kufanyiwa mazishi ya kitaifa.Tunakuuliza maoni yako kuhusu mzozo huo.