Sbs Swahili - Sbs Swahili

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 107:02:25
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Listen to interviews, features and community stories from the SBS Radio Swahili program, including news from Australia and around the world. - Sikiza mahojiano, makala na hadithi za jumuiya kutoka Idhaa ya Kiswahili ya SBS Radio, ikijumuisha taarifa za habari kutoka Australia na ulimwenguni.

Episodios

  • Taarifa ya Habari 30 Mei 2025

    30/05/2025 Duración: 15min

    Wakati inaweza chukua zaidi ya mwaka kwa baadhi ya madai ya bima ya mafuriko kutatuliwa, malipo ya mara moja kwa walio athirika jimboni New South Wales yata anza kutolewa leo 30 Mei 2025.

  • Warudiana tena: mkataba mpya wa upinzani wa mseto baada ya siku nane zaku achana

    30/05/2025 Duración: 08min

    Siku nane baada ya upinzani wa mseto kuachana, vyama vya Liberal na Nationals vime tangaza kuwa vime rudiana tena.

  • Taarifa ya Habari 27 Mei 2025

    27/05/2025 Duración: 16min

    Idadi ya nyumba zilizo haribika kabisa katika mafuriko jimboni New South Wales imeongezeka mara mbili nakufika takriban 800. Huduma ya dharura ya jimbo [[SES]] imesema nyumba 794 katika kanda ya pwani ya kati ya kaskazini, zime zingatiwa kuwa haziwezi tumiwa tena baada ya zaidi ya tathmini 5000 za uharibifu kufanywa.

  • Tafakari, na wito wakuchukua hatua, katika siku ya Kitaifa yakusema Pole

    27/05/2025 Duración: 09min

    Matukio yame fanyika kote nchini Kuadhimisha Siku ya Kitaifa yakuomba msamaha 26 Mei, hatua ambayo ni kukiri kuondolewa kwa lazima kwa watoto wa Mataifa ya Kwanza kutoka kwa familia na tamaduni zao.

  • Taarifa ya Habari 26 Mei 2025

    26/05/2025 Duración: 06min

    Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema hatua ya Israel kuzuia msaada “hai kubaliki kabisa”. Israel ina ruhusu msaada mdogo wakibinadam kuingia Gaza, baada ya takriban miezi mitatu yaku izuia, hali iliyo sababisha uhaba wa chakula na matibabu.

  • UNHCR yaomba msaada kwa wakimbizi wa Sudan Kusini walio DRC

    26/05/2025 Duración: 06min

    Ukosefu wa vyakula na bidhaa zingine muhimu, umelazimisha UNHCR kuomba msaada wa dharura kwa wakimbizi wenye asili ya Sudan Kusini, walio kimbilia DRC.

  • Taarifa ya Habari 22 Mei 2025

    22/05/2025 Duración: 05min

    Kiongozi wa New South Wales, Chris Minns, amesema rasilimali za ziada zinatolewa kwa jumuiya ambazo zime athiriwa kwa mafuriko, katika eneo la kati ya pwaZaidi ya idadi ya watu elfu 48,000 kwa sasa wame tengwa kwa sababu ya maji ya mafuriko.

  • SBS Learn Eng pod 84 Jinsi ya kuelezea uwezo wako waku kimbia (Med)

    22/05/2025 Duración: 14min

    Je, unajua jinsi ya kuzungumzia sifa zako za kukimbia au kufanya riadha?

  • Jinsi ya kufurahia maeneo ya nyika ya Australia kwa kuwajibika

    22/05/2025 Duración: 14min

    Mandhari yakupendaza na tofauti ya Australia, kuanzia pwani hadi jangwani na yote yaliyo katikati, ni nyumbani kwa mimea ya asili na wanyama wakushangaza.

  • Taarifa ya Habari 20 Mei 2025

    20/05/2025 Duración: 17min

    Jimbo la Victoria lina tarajia kupata ziada yake ya kwanza tangu janga la UVIKO-19, wakati serikali ya Allan itakapo toa bajeti ya jimbo hii leo Jumanne 20 Mei 2025.

  • Watu wakujitolea wana jukumu kubwa nchini Australia, ila idadi yao inapungua

    20/05/2025 Duración: 10min

    Wiki ya kitaifa yakujitolea ime anza, ita kuwa kuanzia 19 Mei hadi 25 Mei 2025.

  • Taarifa ya Habari 16 Mei 2025

    16/05/2025 Duración: 15min

    Kiongozi wa Upinzani wa Shirikisho Sussan Ley, amesema kuungana tenana wanawake itakuwa kipaumbele chake kama kiongozi wa Upinzani wa shirikisho.

  • Jeremiah "kuna mkanganyo wa maadili yaki Afrika naya wazungu hapa Melbourne"

    14/05/2025 Duración: 07min

    Baadhi ya wanachama wa jumuiya yawa Afrika wanao ishi Melbourne, Victoria wame kuwa waki kabiliana na wakati mgumu katika kipindi cha kampeni za uchaguzi wa jimbo na shirikisho.

  • Taarifa ya Habari 13 Mei 2025

    13/05/2025 Duración: 17min

    Sussan Ley ame chaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha Liberal. Bi Ley alikuwa Naibu Kiongozi wa chama hicho cha Liberal, alimshinda mpinzani wake mwekahazina kivuli Angus Taylor, katika kura yakumchagua kiongozi mpya muda mfupi ulio pita mjini Canberra.

  • Nafasi za baraza la waziri za tangazwa: Nani yuko ndani, nani yuko nje?

    13/05/2025 Duración: 09min

    Tanya Plibersek ame shushwa cheo nakupewa wizara ya Huduma za Jamii, wakati Anthony Albanese anatangaza baraza lake la mawaziri, atakao fanya kazi nao katika muhula wake wa pili serikalini.

  • Taarifa ya Habari 9 Mei 2025

    09/05/2025 Duración: 18min

    Anthony Albanese akosolewa kwa kumshasha cheo waziri pekee Muislamu katika baraza lake la mawaziri, wakati vyama vya upinzani vya ongeza juhudi yaku wachagua viongozi wao wapya.

  • Adam Bandt akubali kushindwa, asema chama cha Greens kili feli ku kwea mlima Everest

    09/05/2025 Duración: 08min

    Adam Bandt amekubali ameshindwa nakupoteza kiti chake cha Melbourne bungeni, katika matokeo ambayo yame acha chama cha Greens bila kiongozi.

  • Taarifa ya Habari 8 Mei 2025

    08/05/2025 Duración: 06min

    Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema mtazamo wa mhula wa pili wa serikali ya Labor, utakuwa kuimarisha mahusiano na washiriki walio ng’ambo, kuhakikisha utulivu wa kiuchumi nyumbani.

  • Betty afunguka kuhusu jinsi yaku badilisha viza yako ukiwa Australia

    08/05/2025 Duración: 09min

    Wanafunzi wengi wakimataifa wame wasili nchini Australia, kupitia msaada wa mawakala wa uhamiaji.

  • Chama cha Greens cha kabiliana na matokeo yakukatisha moyo katika uchaguzi wa shirikisho

    06/05/2025 Duración: 19min

    Chama cha Greens kina onekana kuwa na viti vichache zaidi ndani ya nyumba ya chini baada ya matokeo ya uchaguzi wa shirikisho wa wikendi iliyo pita ila, wanaweza shikilia usawa wa mamlaka ndani ya Seneti.

página 1 de 26